http://www.ktnkenya.tv
Viongozi katika kaunti ya Makueni wameitaka serikali kuchimba visima vya kutosha na kukarabati visima vilivyoko ili kuwasaidia wakazi kupata maji. Wakiongozwa na mbunge wa Makueni Peter Kiilu, viongozi hao wamesema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakaazi wanaokumbwa na uhaba wa maji . Walizungumza wakati wa kufungua rasmi kisima katika eneo la Nzaui kaunti ya Makueni.