Ni 674 Pekee Kati Ya Takriban Wanafunzi 3,000 Wa Shule Za Upili Na Vyuo Waliojisajili Kupata Ufadhili Wa Masomo Kutoka Kwa Kaunti Waliofanikiwa Kuupata Wadi Ya Gongoni Kaunti Ya Kilifi. Katika Zoezi La Kuwatunuku Waliopata Nafasi Hizo Diwani Wa Eneo Hilo Stephen Baya Alitoa Wito Wa Kuongezwa Kwa Mgao Huo Kutoka Kwa Serikali Kuu Huku Akifichua Kuwa Gavana Wa Kaunti Hiyo Gideon Mung'Aro Alikuwa Ametia Sahihi Mswada Utakaoongeza Mgao Wa Kufadhili Masomo Kutoka Shilingi Milioni 350 Hadi Bilioni Moja.