Uhaba wa mafuta katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa unatatiza shughuli za kawaida katika mji wa Kapsabet kaunti ya Nandi. Mji wa Kapsabet na viunga vyake umeshuhudia uhaba huo na kuwalazimisha madereva wa magari na wahudumu wa bodaboda kulazimika kusafiri mbali hadi kwenye vituo ambavyo vingali na mafuta ili kufanikisha shughuli zao.