Seneti Kukusanya Maoni Ya Wakenya Kuhusu Sheria Tata Ya Vyama

2022-01-11 1

Kamati Ya Seneti Ya Haki Na Sheria Imetwikwa Jukumu La Kukusanya Maoni Ya Wakenya Kuhusu Mswada Tata Wa Mabadiliko Ya Sheria Ya Vyama Vya Kisiasa Na Kuwasilisha Ripoti Yake Katika Kipindi Cha Siku 14. Hii Ni Baada Ya Mswada Huo Kuletwa Mbele Ya Bunge La Seneti Asubuhi Ya Leo Na Maseneta Kueleza Umuhimu Wa Kutwaa Maoni Ya Wakenya. Mswada Huo Tata Ulipitishwa Katika Bungeni Katika Vikao Vilivyosheheni Purukushani.