Kumbukumbu Ya Agnes Tirop

2022-01-05 11

Mshikilizi Wa Rekodi Za Dunia Katika Mbio Za Mita 5000 Na Mita 10000 Letesenbet Gidey Kutoka Ethiopia Na Bingwa Mara Tatu Wa Dunia Katika Nusu Marathon Geofrey Kamworor , Wametoa Ithibati Kushiriki Makala Ya Kwanza Ya Mbio Za Agnes Tirop Memorial World Cross Country Tour Championships Zitakazoandaliwa Februari 12 Huko Kapseret Mjini Eldoret Kaunti Ya Uasin Gishu. Mbio Na Mkondo Utakaotumika Ukizinduliwa Rasmi Jumanne Na Waziri Wa Michezo Dkt Amina Mohammed, Aliyekariri Kujitolea Kwa Serikali Kufadhili Mashindano Hayo Kuhakikisha Yamefana, Kama Njia Ya Kumuenzi Bingwa Wa Zamani Wa Dunia Wa Mbio Za Nyika Agnes Tirop Aliyeuawa Kinyama Na Mumewe Mwaka Uliopita.