Aliyekuwa Rais Wa Nigeria Olesegun Obasanjo Ni Mmoja Kati Ya Wageni Waalikwa Katika Kongamano La Azimio La Umoja Litakaloandaliwa Ijumaa Katika Uwanja Wa Kasarani.
Maandalizi Yamekamilika Huku Waandalizi Wakisema Kuwa Zaidi Ya Magavana 30 Wanatarajiwa Kuhudhuria. Hadi Kufikia Sasa Haijawekwa Bayana Ikiwa Rais Kenyatta Atahudhuria. Odinga Anatarajiwa Kutumia Fursa Hiyo Kutangaza Azma Yake Ya Urais Katika Uchaguzi Wa 2022. Mapema Leo Raila Ailizuru Eneo Hilo Ili Kukagua Maandalizi.