Shule Ya Upili Ya Wasichana Ya Mama Ngina Imefungwa Kwa Muda Usiojulikana Baada Ya Wanafunzi Kujaribu Kuchoma Bweni Mapema Hii Leo. Afisa Wa Elimu Kaunti Ya Mombasa Peter Magiri Amesema Kisa Hicho Kilishuhudiwa Wanafunzi Walipokuwa Wakijiandaa Kwa Masomo Ya Ziada. Wanafunzi Zaidi Ya 1,000 Wameelezwa Nyumbani Huku Uchunguzi Kuhusu Waliopanga Jaribio Ukianzishwa.