Kiongozi Wa Chama Cha ANC Musalia Mudavadi Ameshtumu Vikali Utumizi Wa Gari Za Shule Kwenye Shughuli Za Kibinafsi Kinyume Na Onyo Lililowekwa Na Waziri Wa Elimu Prof George Magoha Aliyetilia Shime Agizo Lililotolewa Na Mtangulizi Wake Dkt Fred Matinag'i. Mudavadi Amedai Kuwa Mabasi Ya Shule Yanatumika Kwa Wingi Kusafirisha Wananchi Kwenye Mikutano Ya Kisiasa Akisema Kuwa Hii Ni Kinyume Na Sheria Zilizowekwa Na Wizara Ya Elimu.