Ruto Akuwa Na Wakati Mgumu Kuhutubia Wakaazi Wa Kondele

2021-11-10 28

Naibu Rais William Ruto Amekuwa Na Wakati Mgumu Kuhutubia Wakaazi Wa Kondele Kaunti Ya Kisumu. Hii Ni Baada Ya Kundi La Vijana Kujaribu Kusambaratisha Mkutano Huo Kabla Ya Kutawanywa Na Vitoa Machozi. Naibu Rais Amenyoshea Kidole Cha Lawama Mrengo Unaongozwa Na Kinara Wa ODM Raila Odinga. Kulingana Na Idara Ya Polisi Kupitia Taarifa Kwenye Vyombo Vya Habari Kisa Hicho Kilichangiwa Pakubwa Na Pesa Za Kampeni.