Mamia Ya Watu Wanasemekana Kukimbia Kutoka Katika Makazi Yao Huku Ghasia Zikizidi Kushamiri Katika Hifadhi Ya Laikipia. Haya Yanajiri Huku Mbunge Wa Zamani Wa Laikipia Kaskazini Mathew Lempurkel Akitiwa Mbaroni Kutoka Nyumbani Kwake Mtaani Ongata Rongai, Kaunti Ya Kajiado Kutokana Na Mapigano Yanayoendelea Laikipia. Mbunge Wa Tiaty William Kamket Pia Amekamatwa Kwa Tuhuma Za Kuhusika Na Machafuko Hayo Ambayo Yanasemekana Kupelekea Vifo Vya Watu 8, Watatu Wao Wakiwa Maafisa Wa Polisi.