Wizara Ya Elimu Imeagiza Shule Ambazo Zilitoza Karo Nje Ya Mwogozo Uliotolewa, Kuwarejeshea Wazazi Fedha Hizo Au Zitumike Katika Karo Ya Muhula Ujao Kwa Wanafunzi Wanaoendelea Na Masomo. Katika Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Iliyotolewa Jumanne, Katibu Katika Wizara Ya Elimu Paul Kibet, Pia Aliagiza Kuwa Hakuna Mwanafunzi Anapaswa Kufukuzwa Shuleni Kwa Kutolipa Karo.