Huku Usajili Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza Ukiingia Siku Yake Ya Tano Hii Leo, Wizara Ya Elimu Imeibua Wasiwasi Kuhusu Idadi Ndogo Ya Wanaosajiliwa Hasa Katika Shule Za Kutwa Za Upili. Waziri Msaidizi Katika Wizara Hiyo Daktari Sara Ruto Amebaini Kuwa Kufikia Alhamisi Tarehe Tano Mwezi Agosti, Shule Za Bweni Zilirekodi Takriban Asilimia 90 Ya Wanafunzi Walioripoti.