Huku Kampuni Ya Kusambaza Umeme Ikilalama Kwa Kukadiria Hasara Kila Mara, Wakenya Kwa Upande Wao Wataendelea Kulipa Mikopo Ya Mabilioni Ya Pesa Kwa Niaba Ya Kampuni Huru Za Uzalishaji Umeme IPPS.Waziri Wa Kawi Nchini Charles Keter Akihojiwa Na Kamati Ya Kawi Katika Bunge La Kitaifa Alifeli Kuwashawishi Wanakamati Wa Bunge Ni Kwa Nini Mwaka Wa Kifedha Wa 2019/2020 Kampuni Ya Kenya Power Ililipa Zaidi Ya Shillingi Bilioni 24 Kwa Kampuni Huru Hata Baada Ya Nyinginezo Kufeli Kuzalisha Na Kusambaza Umeme. Na Kama Mwanahabari Wetu Jeff Khaemba Anavyoripoti Nipe Nikupe Ilishuhudiwa Mbele Ya Kamati Hiyo Ambapo Kila Mmoja Alirushia Lawama Mwenziwe//