Kampuni Ya Maji Ya Malindi Yazindua Teknolojia Ya Kulipia Maji

2021-07-06 3

Wakazi wa Malindi huenda wakapata maji bila matatizo ya hapo awali baada ya kampuni ya maji ya Malindi kuzindua mradi ambao wakazi watalipia maji kabla ya kutumia. Watu 600 tayari wameshawekewa mita 600 za maji katika kijiji cha watamu. Waziri wa maji katika serikali ya kaunti ya Kilifi Kiringi Mwachitu amesema kuwa wizi wa mita utapungua.