Rais Wa Zamani Wa Afrika Kusini Jacob Zuma Kufungwa Gerezani

2021-06-29 6

Aliyekuwa Rais Wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ana Muda Wa Siku Tano Kujisalimisha Katika Kituo Cha Polisi Cha Nyumbani Kwake Nkandla Ama Jijini Johanesburg Ili Kuanza Kifungo Chake Cha Mwaka Mmoja Na Miezi Mitatu Gerezani. Hii Ni Baada Ya Mahakama Kumpata Na Hatia Ya Kukaidi Maagizo Ya Mahakama. Zuma Ambaye Alifurushwa Mamlakani Na Chama Chake Ca Anc Kabla Ya Muhula Wake Kukamilika Alipatikana Na Hatia Baada Ya Kupuuza Agizo La Kufika Mahakamni Kujibu Kesi Ya Ufisadi Iliyokuwa Ikimkabili. Mahakama Ilikuwa Na Jukumu La Kuamua Kama Zuma Alifaa Kuadhibiwa Kwa Kukataa Wito Wa Mahakama Na Amri Ya Mahakama Ya Kumtaka Afike Mahakamani Kutoa Ushahidi Kuhusu Shutuma Za Rushwa Wakati Wa Utawala Wake.