Baadhi Ya Wakenya Wamepinga Vikali Kesi Iliowasilishwa Mahakamani Kuhalalisha Marijuana Maaruf Kama Bangi Hapa Nchini. Kulingana Na Wakenya Tuliowahoji Mitaani Uhalalishwaji Wa Bangi Kutazua Mtafaruku Wa Utovu Wa Nidhamu Na Visa Vya Ujangili Miongoni Mwa Vijana Hapa Nchini. Haya Yanajiri Siku Moja Baada Ya Shirika La Kirastafari Kuwasilisha Kesi Mahakamani Kutaka Uhalalishwaji Wa Bangi Hapa Nchini. Kulingana Nao Bangi Ni Mmea Mzuri Unaotumika Kama Sakramenti Na Waumini Wa Kirastafari Kwenye Ibada Na Vilevile Kama Dawa Kwa Baadhi Ya Magonjwa .