Zaidi Ya Wafanyibiashara 500 Kutoka Katika Soko La Njoro Kaunti Ya Nakuru Wanapania Kuandamana Hadi Katika Afisi Za Kaunti Na Kuwafurusha Maafisa Wake, Kwa Madai Kutelekeza Wajibu Wao. Wafanyibiashara Hao Wanadai Kuwa Licha Ya Kulipa Kodi, Leseni Na Ushuru Bado Wanapata Huduma Mbovu Kutoka Kwa Maafisa Wa Kaunti Kama Vile Mazingira Duni Yenye Uchafu Na Ukosefu Wa Choo, Maji Safi Na Ukosefu Wa Usalama Kwa Ujumla.