Wabunge Walalamikia Njama Ya Serikali Kuagiza Sukari Kutoka Uganda

2021-04-28 10

Wabunge Kutoka Maeneo Ya Ukuzaji Miwa Wamelalamikia Njama Ya Serikali Kupanga Kuagiza Sukari Kutoka Mataifa Ya Kigeni Huku Viwanda Vya Kusaga Miwa Nchini Vikididimia .Wabunge Hao Wamenyoshea Lawama Serikali Kuwa Chanzo Cha Masaibu Yanayokumba Sekta Ya Ukuzaji Miwa.Wakiongozwa Na Mbunge Wa Muhoroni Onyango Oyoo, Johnson Naica Wa Mumias West, Tom Odege Wa Nyatike Na Jared Otieno Wa Nyando Wamesema Ipo Haja Kwa Serikali Kufufua Viwanda Vya Sukari Na Vilevile Kukumbatia Mchango Wake Badala Ya Kuagiza Sukari Kutoka Mataifa Mengine Hatua Wanayohofia Italemaza Na Kuyumbisha Sekta Ya Sukari