Kikosi Cha Makachero Kimeanzisha Msako Dhidi Ya Mbunge Wa Malindi Aisha Jumwa Anayesemekana Kuingia Mafichoni Baada Ya Mkurugenzi Wa Mashtaka Ya Umma Noordin Haji Kuidhinisha Kukamatwa Kwake. Katika Taarifa Yake Mkurugenzi Mkuu Wa Mashtaka Ya Umma Noordin Haji Aliamuru Kukamatwa Kwa Jumwa Na Kufunguliwa Mashtaka Kuhusiana Na Matumizi Mabaya Ya Kima Cha Shilingi Milioni 19 Fedha Za Ustawi Wa Maeneo Bunge.