Wafanyikazi Wa Kaunti Ya Nairobi Waandamana Nje Ya Ofisi Ya Gavana

2020-07-27 138

Baadhi ya wafanyikazi wa kaunti ya Nairobi wameandamana nje ya ofisi ya gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko wakilalamikia kucheleweshwa mishahara yao. Wafanyikazi hao wanasema kuwa hawajalipwa miezi mitano hali ambayo imesababishwa na sintofahamu ya uongozi wa kaunti ya Nairobi baada ya rais Uhuru Kenyatta kuteua Generali Mohamed Badi kama mkurugenzi wa NMS.