Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"(Official Video)
Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake."
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.
Barua Pepe: contact.sw@kingdomsalvation.org
Wasiliana Nasi: +254-700-427-192