Kupitia #TheTrends
Msanii mkubwa wa filamu nchini Nigeria, Van Vicker, amewasili nchini saa 10 Alfajiri leo na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ni msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu. Van Vicker amekuja nchini kwa ajili ya kuzindua filamu yake aliyofanya na Wema inayoitwa 'D.A.D' ambayo itazinduliwa Katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Septemba 28 ambapo pia itakuwa ni siku ya kuzaliwa ya Wema Sepetu
Msanii Huyo Van Vicker Amefunguka Juu Ya Wasanii Anaokubali Kazi Zao Tanzania Akiwemo Wema Sepetu.