Mshukiwa akamatwa kuhusiana na kifo cha Monica Kimani

2018-09-26 1

Mshukiwa wa mauaji  ya mwanamke mmoja  kwa jina Monica Kimani aliyepatikana ameuwawa kinyama nyumbani kwake mtaani Kilimani Alhamisi iliyopita amekamatwa na polisi. 

Mshukiwa huyu kwa jina Joseph Kuria Irungu  alikamatwa na polisi leo saa kumi alfajiri baada ya taarifa yake kuhitilafiana na madai yake kuwa, alikuwa amepigwa risasi na wezi siku ambayo mwanamke huyo aliuwawa, na badaye polisi katika eneo la Lang'ata kukosa ushahidi wa kutosha kuhusiana na tukio hilo.

Kama anavyotuarifu  Angela Cheror mshukiwa huyo amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani, huku uchunguzi zaiadi ukiendelea.