Viongozi kutoka kaskazini mwa Kenya wameungana pamoja kwenye hafla ya kuchangisha pesa zitakazogharamia matibabu ya iddris mukhtar aliyepigwa risasi tatu kichwani wiki tatu zilizopita na angali kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Aden Duale aidha amewaomba wakenya kuzipa taasisi za uchunguzi muda ili kutekeleza majukumu yao kuambatana na suala hilo.
Jumla ya shilingi milioni kumi na sita zilichangishwa kwenye hafla hiyo huku Gavana Ali Korane akituma mchango wake binafsi wa shilingi milioni mbili.
Korane amekuwa mshukiwa wa shambilizi hilo mnamo mwezi uliopita ikisemekana kwamba Mukhtar alikuwa ametilia shaka vyeti vya masomo vya gavana huyo.