Watu 4 wafariki baada ya kula kitoweo cha sumu Bungoma

2018-09-15 1

Watu wanne wamefariki katika eneo la Mlima Elgon, baada ya kula uyoga almaarufu mushroom, unaosemekana kuwa na sumu.

Wanne hao waliofariki ni mama na mwanawe pamoja na jirani na jamaa mwengine.

Wanne hao waliodaiwa kuaga dunia baada ya kula uyoga huo wa sumu ni mama na mtoto wake, na watu wengine wawili huku mmoja akidaiwa kuwa raia wa nchi jirani ya Uganda.

Aidha kisa hicho kimewashangaza wengi huku wenyeji wa eneo hilo wakijiuliza inakuwaje kitoweo mama alichowaandalia wanawe kuwa sumu iliyomuangamiza yeye pamoja na familia yake