Tundu Lissu ataja Mambo matano(5) Mazito

2018-08-29 12

Ni Takriban miezi minane sasa tangu mwanasiasa wa upinzani na Mbunge wa Singida Mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu kuwepo nchini Ubelgiji kwa ajili ya kupata matibabu. Mbunge wa upinzani Tundu Lissu anasema bunge la Tanzania halijajikimu kulipa gharama za matibabu yake tangu alazwe hospitalini. Hatahivyo serikali kwa upande wake imeeleza kuwa Bwana Lissu hakufuata utaratibu unaotakiwa wa kupelekwa kwanza katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ili aweze kuandikiwa mapendekezo ya kupelekwa na kutibiwa nje ya nchi au katika hospitali nyingine. Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ameiambia BBC Dira ya Dunia kwamba iwapo utaratibu huo utafuatwa hata sasa, malipo ya huduma zote za matibabu zitalipwa na bunge la Tanzania.

Katika mazungumzo yake na mwandishi wa BBC, Zuhura Yunus ambaye alimtembelea hosptalini ,Tundu Lissu alibainisha hali ya upinzani nchini Tanzania kuwa ina mabadiliko makubwa tofauti na miaka ya nyuma.

Free Traffic Exchange