Kilichomtokea RAIS JPM MSIBANI KWA MZEE MAJUTO KINAHUZUNISHA,ASHINDWA KUJIZUIA NA KUMWAGA MACHOZI

2018-08-10 4

Rais Dokta John Pombe Magufuli,meshindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akimwaga machozi kutokanana huzuni aliyokuwa nayo, wakati akiaga mwili wa marehemu Amri Athuman 'King Majuto' katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
#RAIS_MSIBANI #MAGUFULI _MZEE_MAJUTO

Mwili wa msanii mkongwe wa filamu za Kibongo, Amri Athuman 'King Majuto', aliyefariki jana usiku, umetolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ulikokuwa umehifadhiwa, na kupelekwa kuswaliwa katika Msikiti wa maamur, Upanga kisha katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa.

Baada ya kuagwa katika Viwanja vya Karimjee, mwili wa marehemu utasafirishwa mpaka jijini Tanga kwa mazishi ambapo viongozi mbalimbali wamejitokeza kushiriki katika msiba huo.