JPM afika nyumbani kwa JK kutoa Pole

2018-07-21 2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli tarehe 21 Julai 2018 ameenda kutoa pole kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Mkwewe Mzee Rashid Mkwachu Msasani jijini Dar es salaam.

Marehemu Mzee Mkwachu ambaye ni baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete,aliyefariki dunia tarehe 19 Julai 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini DSM

Mheshimiwa Dkt. Magufuli ameongozana na mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli