Historia ya 'PROF MAJI MAREFU' Kutoka UGANGA Hadi UBUNGE!
Steven Hilary Ngonyani au maarufu kama Maji Marefu, aliyekuwa Mbunge wa Korogwe vijijini hatunaye tena duniani baada ya kufikwa na mauti Julai 2, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akiendelea na matibabu.
Kifo cha Profesa Maji Marefu kimetokea wiki chache baada ya mkewe, Mariam kufariki ambaye kama ilivyo kwa Profesa Maji Marefu, naye alifia katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Tofauti na wanasiasa wengi, historia ya Profesa Maji Marefu ipo tofauti kidogo.
Uprofesa wake haukutokana na kusoma kama walivyo maprofesa wengi ndani na nje ya nchi, bali ulitokana na uwezo na utaalamu wa hali ya juu katika fani ya uganga wa kienyeji.
Kabla hajawa mwanasiasa, Profesa Maji Marefu alikuwa mganga wa kienyeji na mwanamazingaombwe maarufu, ambaye alikuwa akifahamika sana ndani na nje ya nchi kutokana na kazi zake za uganga.
Inaelezwa kwamba hata jina lake la Maji Marefu, lilitokana na uwezo aliokuwa nao katika kupambana na wachawi na watu waliokuwa wakitumia nguvu za giza vibaya kuwadhuru wengine.
Umaarufu wake ulikuwa mkubwa kwenye miaka ya 1990 ambapo alikuwa akisafiri mpaka nchi za mbali, ikiwemo Falme za Kiarabu kwenda kuwatibu watu waliokuwa na matatizo mbalimbali, kama majini, kurogwa, kufungwa nyota na maradhi yaliyokuwa hayaonekani hospitalini.
Ni katika kipindi hicho pia alikuwa akizunguka kwenye shule za msingi na sekondari nchi nzima, akionesha michezo ya mazingaombwe kwa wanafunzi na walimu, kazi iliyompa umaarufu mkubwa.
Profesa Maji Marefu alizaliwa Mei 25, 1956 Korogwe Vijijini mkoani Tanga ambapo baadaye, mwaka 1970 alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kwamndolwa, Korogwe.
nstall GlobalPublishersApp Android: iOS: Subscribe FACEBOOK: ... TWITTER: Visit
, Subscribe Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
WEBSITE: FACEBOOK: ... TWITTER: INSTAGRAM: ..