Maajabu ya Jeneza la Maria na Consolata

2018-06-06 2

Maajabu ya Jeneza la Maria na Consolata

ZOEZI la uchimbaji wa kaburi kwa ajili ya maziko ya mapacha walioungana, marehemu Maria na Consolata limefanyika katika Makaburi ya Masista wa Shirika la Bikira Maria wa Consolata Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa leo Jumanne, Juni 5, 2018.

Wananchi walio wengi wamejitokeza kuandaa nyumba ya milele ya mapacha hao walioaga dunia usiku wa Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa walikokuwa wakitibiwa.

Aidha, mafundi katika Kampuni ya Mandela wamefanya maandalizi ya mwisho ya utengenezaji wa jeneza litakalotumika kuwazikia mapacha haao.

Shughuli ya kuandaa jeneza hilo imefanyika katika eneo la Sido Manispaa ya Iringa, kama picha zinavyoonyesha.

Mazishi ya mapacha hao yanatarajjwa kufanyika kesho Jumatano kwenye makaburi ya Masista Tosamaganga mkoani Iringa.

Instal GlobalPublishersApp Android: iOS: Subscribe FACEBOOK: ...

TWITTER: Visit , Subscribe

kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… WEBSITE: FACEBOOK: ... TWITTER: INSTAGRAM: ..