Gospel Movie Video Swahili "Ivunje Laana" (4) - Je, Imani katika Biblia Ni sawa na Imani katika Bwana?

2018-05-16 3

Wachungaji wengi sana na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini huamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana, na kwamba kuamini katika Bwana ni kuamini katika Biblia, na kuamini katika Biblia ni kuamini katika Bwana. Wao huamini kwamba mtu akiachana na Biblia basi hawezi kuitwa muumini, na kwamba mtu anaweza kuokolewa na anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni almradi ashikilie Biblia. Je, Bibilia inaweza kweli kumwakilisha Bwana? Je, uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi hasa? Bwana Yesu alisema, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai" (Yohana 5:39-40). Mwenyezi Mungu alisema, "Hata hivyo, kipi ni kikubwa? Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? … Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?" (Neno Laonekana katika Mwili)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Injili ya Kushuka kwa Ufalme: https://sw.kingdomsalvation.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu: https://sw.godfootsteps.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu YouTube: https://www.youtube.com/channel/UCkUDnudSY6_KR123N2Yr7mw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Facebook: https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Twitter: https://twitter.com/CAGchurchsw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Instagram: https://www.instagram.com/thechurchofalmightygodsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Vimeo: https://vimeo.com/thechurchofalmightygodsw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Blogger: http://nikanisalamwenyezimungu.blogspot.com/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Wordpress: https://nikanisalamwenyezimungu.wordpress.com