RAIS MAGUFULI AMUOKOA LULU, JESHI LA MAGEREZA LATOA KAULI

2018-05-15 1

MAGEREZA WASEMA LULU ‘AMETOKA’ KWA MSAMAHA WA RAIS

Msanii nyota wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu, ameachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Magufuli, alioutoa kwa wafungwa katika Sikukuu ya Muungano Aprili 26, mwaka huu.

Hata hivyo, msamaha wa rais kwa msanii huyo ambaye ameachiwa Jumamosi wiki iliyopita, ni kubadilishiwa au kupunguziwa adhabu kutoka kifungo cha miaka miwili alichokuwa akitumikia hadi kifungo cha nje ambacho atamaliza Novemba 12, mwaka huu.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatatu Mei 14, Naibu Kamishna wa Magereza, Augustino Mboje amesema Magereza ilipokea amri kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kwamba mfungwa huyo amebadilishiwa adhabu hivyo wamwachie huru.

Usipitwe na Matukio Muhimu kila siku na taarifa za Habari Mubashara yaani Live kila siku kwenye Channel hii. Subscribe sasa na bofya alama ya kengere inayotokea baada ya Subscribe. Fungua Link hii .