MTIBWA SUGAR 0-1 SIMBA SC: FULL HIGHLIGHTS (VPL 09/04/2018)

2018-04-12 5

Mechi imemalizika kwa ushindi mwembamba upande wa Simba licha ya kushambuliwa zaidi hasa dakika za mwisho kipindi cha pili.

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ameifungia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukipigwa katika dimba la Jamhuri, Morogoro.

Katika mchezo huo mgumu na uliokuwa na ushindani mkali, bao la Simba lilipatikana dakika ya 24 ambapo kinara huyo wa mabao aliunganisha pasi ya kichwa ya kutoka kwa John Bocco, baada ya kros ya Shiza Kichuya kutoka upande wa kushoto.

Baada ya mchezo huo umati mkubwa ulionekana kujaa katikati ya dimba.

Mchezo ulivyokuwa....