VICHWA VYABAKI NA MASWALI KIFO CHA MFANYABIASHARA WA MABASI JIJINI MWANZA

2018-03-17 5

HATIMAYE mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa mabasi jijini Mwanza Samson Josiah ambaye alikuwa mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya abiria ya Super Sami, umezikwa leo katika makaburi ya kikristo yaliyoko wilayani Magu mkoani Mwanza.

Majira ya saa 9:30 alasili mwili wa mfanyabiashara huyo ulishushwa na kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele ikiwa ni mara baada ya ibada ya mazishi iliyotangulia ikiongozwa na Mchungaji Jackson Meza kutoka Kanisa la African Inland Church of Tanzania (AICT) kufanyika nyumbani kwake alikokuwa akiishi mtaa wa Majengo Mapya wilayani Magu.

Kwaya ya kanisa ambayo marehemu alikuwa mfadhili wake iliimba nyimbo za maombolezo zenye hisia na hata kusababisha maelfu ya wa waombolezaji wamemiminika kutoka sehemu mbalimbali kuangua kilio kwenye ibada hiyo.

Hata hivyo mwili wa marehemu Josiah haukuweza kufunguliwa katika jeneza lake na kuagwa kwa njia za kawaida kama zilivyo taratibu za imani ya kikristu kutokana na taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu kusema kuwa mwili wa ndugu yao ulikuwa umeharibika sana.

Jembe Fm kupitia mwanahabari wake Albert G. Sengo imefanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Jafar Mohamed:-