Cheche, mpiga picha, anabahatika kuzawadiwa studio ya kizamani ya biashara, na marehemu Habibu, mpiga picha maarufu na wa kipekee.\r
\r
Lakini si wote wanaoridhika kuwa ile ni bahati. Dafu, rafiki yake, ambaye ni fundi umeme, anatishwa sana na jengo lile. Mwanaidi, mama mkwe wake, ana uhakika kuwa Cheche hatopata pesa za kutosha kwenye biashara hii mpya, kumudu kumtunza mke wake kijana, Cheusi, ambaye tayari ana ujauzito wa mtoto wa tatu. Hapohapo Cheche anajirusha na Tula, mwandani wake wa ujanani, anayemiliki kigrosari kidogo.\r
\r
Mjini nako, Duma, kijana mwenye haiba ananunua vifaa vya wizi kwa ajili ya biashara yake ya kutumbuiza na muziki. Wakati rafiki yake wa kike, Nusura anapokwenda kupiga picha kwenye studio mpya, analazimika badala yake kumpiga picha baba yake Cheusi, Mzee Kizito mwenye wake wengi na familia kubwa. Ni nani angejua kuwa huu ni wasaa wa kudura? \r
\r
-------------------------------------\r
\r
Photographer Cheche gets lucky when he is gifted an old commercial studio by the late, Habibu, a well-known and eccentric photographer.\r
\r
But not everyone is convinced that its good luck. His friend, Dafu, an electrician, is spooked by the old building. Cheches mother-in-law, Mwanaidi, is also sure that Cheche wont make enough money from this new business to support his young wife Cheusi, already pregnant with a third child. In any case, Cheches playing games with his teenage sweetheart, Tula, who runs a little kigrosari \r
\r
Across town, good-looking Duma buys a shipment of stolen equipment for his deejaying and music business. When his girlfriend, the beautiful Nusura turns up at the new studio to have her photo taken she has to take a picture instead of Cheusis father, Mzee Kizito, a polygamist and big family patriarch. Whos to know its a moment of destiny?\r
\r
-----------------\r
\r
Swahiliwood.com ni tovuti ya video ya kwenye mtandao iliyo rasmi kwa vipindi vya kiswahili. Kuanzia documentary mpaka maigizo, ucheshi na vipindi vingine vya runinga. Tunakuletea kiwango cha juu cha ubora wa burudani za Kiswahili kutoka Afrika Mashariki kwa Afrika Mashariki.\r
\r
Bongo Filamu